Kujifunza kwa Furaha, Kukua kwa Imani

Tunayo furaha kubwa kukukaribisha kwenye Idara ya Watoto, mahali ambapo mioyo midogo inakutana na upendo wa Yesu Kristo kwa njia ya furaha na mafundisho. Katika idara hii, tunatumia mbinu za kipekee kama michezo (Games) na hadithi za Biblia ili kuwafundisha watoto Neno la Mungu kwa njia rahisi na yenye kuvutia.

Lengo letu ni kuwajengea watoto msingi wa kiroho unaowawezesha kumjua Yesu Kristo, kuwa na maadili bora, na kukua wakiwa wafuasi wa kweli wa Bwana. Hapa, watoto wanapata fursa ya kushiriki, kujifunza, na kufurahia safari ya kiroho kwa pamoja.

Games Za Kikristo

Tunayo furaha kukukaribisha katika sehemu maalum ya tovuti yetu iliyoandaliwa kwa ajili ya watoto. Hapa, watoto wako wanaweza kucheza michezo ya Kikristo iliyoundwa kuwafundisha maadili ya Biblia kwa njia ya kufurahisha na yenye kuvutia.

Michezo hii ni fursa ya kipekee ya kuwasaidia watoto wako kumjua Yesu Kristo, kuimarisha imani yao, na kukuza maarifa yao ya Neno la Mungu kupitia burudani yenye mafundisho mazuri. Unapomsimamia na kumsapoti mtoto wako, unachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza msingi wake wa kiroho na maadili.