Familia Yako ya Kiimani

Tunapenda kukukaribisha kwa moyo mkunjufu katika Familia Media, chombo cha habari kinachomilikiwa na KKKT-DMP-Kifuru. Hapa ni mahali ambapo upendo, tumaini, na imani vinaungana kwa ajili ya kuhamasisha na kubadilisha maisha.


Kupitia vipindi vyetu, tunalenga kuhubiri Injili, kushirikisha ushuhuda wa kutia moyo, na kutoa mafundisho yanayokuimarisha katika safari yako ya kiroho. Kama sehemu ya familia hii, tunakuunganisha na jamii yenye lengo la kueneza mwanga wa Kristo na kujenga kizazi bora kinachoongozwa na maadili ya Kikristo.

Vipindi Kwa Ajili Yako

SAFARI YA IMANI

Safari ya Imani ni kipindi maalum kinachotupa fursa ya kusikiliza shuhuda za kutia moyo na kuimarisha imani zetu. Kupitia vipindi hivi, tunawasikia ndugu zetu waliokutana na changamoto mbalimbali, wakashinda kwa neema ya Mungu. Ushuhuda wao unathibitisha nguvu ya imani na matumaini katika Kristo

MPANGO Mkakati

Kipindi cha Mpango Mkakati kinatualika kukutana na wafanyabiashara, viongozi wa taasisi, na wataalamu mbalimbali. Hapa tunajifunza mbinu na mikakati bora ya kupanga na kutekeleza mipango inayozalisha matokeo. Lengo ni kupata maarifa ya kutufanikisha katika huduma na maisha yetu ya kila siku.

NENO LA UZIMA

Neno la Uzima ni mfululizo wa mahubiri yanayotolewa na watumishi wa Mungu kutoka ndani na nje ya Kanisa. Kipindi hiki kinahusu kujenga imani yako kupitia mafundisho yenye nguvu ya Neno la Mungu. Ni nafasi ya kupata chakula cha kiroho kinachokupa ujasiri wa kusonga mbele katika safari ya wokovu.

MWANAMKE NA MAISHA

Mwanamke na Maisha ni kipindi cha majadiliano kinacholenga kumulika mchango wa mwanamke katika maendeleo ya familia, jamii, na taifa kwa ujumla. Kupitia mazungumzo haya, tunajadili changamoto, fursa, na njia bora za kumwezesha mwanamke kufanikisha maisha yake na ya watu wanaomzunguka.

Tuzungumze Afya

Tuzungumze Afya ni kipindi kinacholenga kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya afya ya mwili, akili, na roho. Kupitia kipindi hiki, tunajadili njia bora za kuishi maisha yenye afya, kukabiliana na changamoto za kiafya, na kuimarisha ustawi wa familia na jamii.

Tunakaribisha wataalamu wa afya, waganga wa tiba asilia na tiba ya kisasa, pamoja na watu waliopitia changamoto za kiafya, kushiriki maarifa yao. Lengo kuu ni kukuza ufahamu na kuhimiza hatua za kinga na matibabu ili kufanikisha maisha bora kwa wote.

Kona ya Tafakari ya Neno