Karibu Kanisani

Karibu KKKT-DMP-KIFURU

Mtaa wa Kifuru ni miongoni mwa Mitaa inayolelewa na Usharika wa Segerea. Mtaa huu upo katika Wilaya ya Ilala umbali wa kilomita 5 kutoka Kinyerezi kwa kupitia barabara ya Kinyerezi hadi Mbezi kupitia Marambamawili. Mtaa huu ulianza mnamo mwaka 2008 na ulianza ukiwa na Wakristo 9; mpaka sasa mtaa una washarika takribani 800

Lengo Kuu

Lengo kuu la KKKT ni kuwapa watu nafasi ya kumfahamu Yesu Kristo ili wapate uzima wa milele. Kanisa hili limejengwa juu ya msingi imara wa Yesu Kristo, likiongozwa na Neno la Mungu kama lilivyoandikwa katika Agano la Kale na Agano Jipya (Biblia ya Kikristo), na linaimarishwa kupitia sakramenti takatifu.

Kupitia mafundisho, huduma, na ushuhuda wake, KKKT inalenga kueneza Injili kwa ujasiri, huku ikijenga jamii yenye upendo, matumaini, na mshikamano wa kweli kwa utukufu wa Mungu.

Utume

Kuwafanya watu wamfahamu Yesu Kristo na kupata uzima kamili kwa kuwafikishia Habari Njema kupitia maneno na matendo, kwa misingi ya Neno la Mungu kama lilivyo katika Biblia na mafundisho ya Kilutheri yanayoongozwa na Katiba ya KKKT.

Tunu Za Msingi

Kupitia Upendo, Maombi, Uwajibikaji, Umoja, na Heshima, tunajifunza kuishi kwa mfano wa Yesu Kristo na kueneza Neno Lake kwa maneno na matendo. Tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu ujifunze zaidi kuhusu maadili haya na jinsi yanavyotuimarisha kiimani na kijamii.

Karibu, utafakari nasi msingi wa imani yetu!

Upendo

“Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.”
(Mathayo 22:37-39)

Maombi

“Kwa hiyo nawaambia, chochote mtakachoomba mkisadiki kwamba mmepokea, mtapewa.”
(Marko 11:24)

Uwajibikaji

“Mtu na atufikirie hivi: sisi ni watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Na zaidi ya hayo, inahitajika katika mawakili mtu awe mwaminifu.”
(1 Wakorintho 4:1-2)

Umoja

“Ili wote wawe na umoja, kama vile Wewe, Baba, ulivyo ndani Yangu, nami ndani Yako, ili nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kusadiki kwamba Wewe ndiwe Uliyenituma.”
(Yohana 17:21)

Heshima

“Lakini haki na itiririke kama maji, na haki kama kijito cha daima.” (Amosi 5:24)