Ratiba ya Kanisa Ndani ya Juma
Maswali yaulizwayo
Tunayo furaha kukukaribisha kwenye sehemu ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs). Hii ni sehemu maalum iliyoundwa kukupa majibu ya haraka kwa maswali yanayohusiana na Kanisa la KKKT-DMP-Kifuru, huduma zetu, na taratibu mbalimbali.
Tunalenga kufanya uzoefu wako kuwa rahisi na wa manufaa, iwe ni kuhusu jinsi ya kujisajili kama msharika, kujiunga na vikundi vya huduma, au kutafuta msaada wa kiroho. Ikiwa huwezi kupata jibu la swali lako hapa, tafadhali wasiliana na ofisi ya Kanisa kwa msaada zaidi.
Unaweza kujisajili rasmi kuwa msharika wa Kanisa kwa kutembelea tovuti yetu ya usajili kupitia usajili.lutherankifuru.org. Fuata maelekezo yaliyopo kwenye tovuti ili kukamilisha usajili wako.
Tafadhali fika ofisi ya Kanisa ili kupatiwa utaratibu wa jinsi ya kuwa Mkristo. Watumishi wetu wa kiroho watakuelekeza hatua muhimu na kukusaidia katika safari yako ya imani.
Kanisa linapatikana eneo la Kifuru, njia ya kwenda Stesheni ya Treni Pugu. Tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi ya kufika.
Wakati wa kujisajili kama msharika kupitia tovuti yetu au kwa ofisi ya Kanisa, kuna sehemu ambayo unaweza kuchagua idara au kikundi unachotaka kujiunga. Vikundi hivi ni pamoja na kwaya, vikundi vya maombi, na idara za huduma mbalimbali.
Wakati wa kujisajili kama msharika kupitia tovuti yetu au kwa ofisi ya Kanisa, kuna sehemu ambayo unaweza kuchagua idara au kikundi unachotaka kujiunga. Vikundi hivi ni pamoja na kwaya, vikundi vya maombi, na idara za huduma mbalimbali.
Madarasa ya Kipaimara huanza kila Januari. Tafadhali fika ofisi ya Kanisa mapema ili upate fomu ya usajili na ratiba ya mafunzo kwa ajili ya mtoto wako. Kanisa, kuna sehemu ambayo unaweza kuchagua idara au kikundi unachotaka kujiunga. Vikundi hivi ni pamoja na kwaya, vikundi vya maombi, na idara za huduma mbalimbali.
Ndiyo, Kanisa linatoa huduma za kiroho kama harusi, ubatizo, mazishi, na baraka za familia. Tafadhali wasiliana na ofisi ya Kanisa ili kupanga na kupatiwa msaada unaohitajika.
Sadaka na michango ya hiari kwa Kanisa zinaweza kutolewa kupitia akaunti rasmi ya Kanisa
KKKT-KIFURU
047042926021
MaendeleoBank
au kupitia namba ya M-PESA lipa namba
5440839.
Tafadhali fika ofisini au wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.
Ndiyo, Kanisa lina miradi na programu mbalimbali kwa vijana na watoto, kama vile mafunzo ya uongozi, vikundi vya maombi, na huduma za watoto. Tafadhali jiunge na programu hizi ili kukuza imani yako na kushirikiana na wengine.
Ndiyo, tunarusha baadhi ya vipindi vya ibada na mafundisho kupitia chombo cha habari cha Kanisa. Angalia ratiba yetu ya matangazo kwenye tovuti au ukurasa wetu wa mitandao ya kijamii.
Ndiyo, tunatoa ushauri wa kiroho, kifamilia, na hata kwa vijana wanaokabiliana na changamoto za maisha. Fika ofisini au panga muda wa kukutana na mchungaji kwa msaada huu.
Unaweza kuwasiliana na ofisi ya Kanisa kwa simu 0713 450 450, barua pepe, au kufika moja kwa moja. Timu yetu iko tayari kukusaidia kwa maswali yoyote au mahitaji yako.