Miradi

Miradi Yenye Tija-2025

Kama sehemu ya juhudi za kuchochea maendeleo ya kiroho na binafsi kwa washarika wetu, Kanisa linabuni na kutekeleza miradi yenye tija inayolenga kuboresha maisha ya kiroho, kijamii, na kiuchumi.
Miradi hii inalenga kuimarisha mshikamano wa jamii ya waumini, kukuza imani, na kuandaa mazingira bora ya utumishi kwa Mungu. Tunakukaribisha kushirikiana nasi katika kufanikisha maono haya makubwa kwa utukufu wa Mungu.