Kujifunza, Kuhudumu, na Kuleta Mabadiliko

Tunayo furaha kubwa kukukaribisha katika Idara ya Umoja wa Wanawake, mahali ambapo wanawake wanakuja pamoja kwa upendo, mshikamano, na maono ya kipekee ya kuleta mabadiliko chanya katika familia, Kanisa, na jamii kwa ujumla.

Idara hii imejikita katika kutekeleza shughuli mbalimbali zenye lengo la kujenga maisha ya kiroho, kijamii, na kiuchumi.

Mwanamke na Maisha

Mwanamke na Maisha ni kipindi cha majadiliano kinacholenga kumulika mchango wa mwanamke katika maendeleo ya familia, jamii, na taifa kwa ujumla. Kupitia mazungumzo haya, tunajadili changamoto, fursa, na njia bora za kumwezesha mwanamke kufanikisha maisha yake na ya watu wanaomzunguka.

Matangazo Idara ya Wanawake